MAN U: Unafahamu kuwa Moyes alikuwa bora zaidi ya Farguson?
https://videozasoka.blogspot.com/2014/05/man-u-unafahamu-kuwa-moyes-alikuwa-bora.html
Katika takwimu zilizofanywa na wapenzi wa soka nchini uingereza zinaonesha kuwa David Moyes alikuwa na mafanikio katika mechi zake za mwanzo akiwa kama kocha wa timu ya Man U zaidi ya alivyokuwa Sir Alex Farguson, Takwimu zinaonesha kuwa katika mechi 31 za mwanzo alizo kiongoza kikosi cha Man u, alishinda jumla ya mechi 18, akatoa sare mechi 6 na kupoteza mechi 7 wakiti Fargie alishinda mechi 12 akatoa sare mechi 10 na kupoteza mechi 9.
Hivyo kuonekana kuwa uongozi wa Man U haukumtendea haki kwa kutokuweza kumvumilia. Hata hivyo moyes atalipwa kiasi cha £5m ambacho ni sawa na Tshs 1,389,593,600 tofauti na ilivyofikiriwa hapo awalikuwa angelipwa mshahara wote wa mkataba wake wa miaka 6. Hata hivyo kiasi hicho kinampa uhuru wa kufauta ajira katika kikosi kingine chochote tofauti navile ambavyo angelipwa mshahara wa miaka sita na kulazimishwa kukaa bila kutafuta ajira sehemu nyingine.
Tetesi zinaonesha kuwa kuna dalili za Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal anapewa nafasi kubwa katika kuirithi mikoba ya David Moyes.
